The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Ujumbe wa Katibu wa Mufti

Nina furaha ya kukukaribisha katika tovuti ya Ofisi ya Mufti Zanzibar, tunatumai utapata habari zenye kuaminika na zilizo kamili zitakazo kupa muungozo kuhusu dira, dhamira, shughuli na lengo kuu la Ofisi ya Mufti Zanzibar.

Lengo kuu la tovuti hii ni kufikia miongoni mwa matarajio ya Ofisi ya Mufti ya kutoa fatwa, miongozo ya kidini na kusimamia masuala yote ya kiislamu kwa mujibu wa Sheria ya Mufti Namba 9 ya Mwaka 2001. Tovuti hii inatarajia kuendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na mikakati  inayochukuliwa na Ofisi ya Mufti katika  utoaji wa miongozo ya kitaifa ya kiislamu, kuimari sha uadilifu, ubora na ufanisi katika utoaji wa fatwa, utatuzi wa migogoro na usimamizi wa masuala ya kiislamu.

 Ni matumaini yangu kwamba tovutihii itakua ni bora na yenye kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, Nia yetu ni kuboresha tovuti hii kila baada ya muda ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma kwa wananchi wote wa Tanzania na wageni wandani na nje ya nchi.

Shukrani

Katibu wa Mufti wa Zanzibar

Ofisi ya Mufti

Zanzibar