The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Habari

Matukio

Karibu katika Tovuti ya Mufti wa Zanzibar

Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1992 kwa Amri ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa wakati huo Mhe. Dk.Salmin Amour Juma. Aidha, baadae ikaanzishwa upya kwa Sheria ya Mufti Namb. 9 ya mwaka 2001. Kabla ya kuanzishwa  Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar baadhi ya kazi za msingi zilikuwa zikifanywa na Mashekhe mbali mbali wakiwemo wale wa Msikiti Gofu, wakiwemo Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Fatawi bin Issa n.k ambao walikuwa wakitoa Fatwa mbali mbali, utatuzi wa migogoro na kutoa Miongozo mbali mbali kwa kadri ilivyohitajika kwa wakati huo.  Ama kwa upande wa Serikali, Mahkama ya Kadhi Mkuu ilikuwa ikitumika kwa madhumuni hayo.

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِفَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُون

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. “Qur-an 4:103”