The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Huduma Zetu

HUDUMA KWA WATEJA KATIKA OFISI YA MUFTI ZANZIBAR

Huduma zetu ni nzuri na nizabure na zinajali jamii yote.

Ofisi ya Mufti inatoa huduma kwa jamii, huduma zinazotolewa ni Usajili wa Misikiti, Madrsa, Kusilimisha wasiokua waislamu, Kuendesha mafunzo ya ndoa, kutoa fatwa katika mambo mbalimbali ya kiislamu , kusuluhisha migogogoro ya ndoa na kutoa mafunzo ya ualimu kwa Waalim wa Madrasa.

Utaratibu wa Usajili wa Misikiti/Madrasa

Kabla ya kufika Ofisi ya Mufti, muhusika anatakiwa kwanza aandike barua yake yenye kichwa cha habari ya ombi la kusajili Msikiti/Madrsa.

Katika barua hiyo anatakiwa aeleze habari zote muhimu zinazo jitosheleza na ombi lake la Msikiti/Madrasa

USAJILI WA MISIKITI

Katika ombi la usajili wa Misikiti Mteja anatakiwa  ataje jina la msikiti wake, pahala ulipo, Shehia, Wilaya na Mkoa. Aeleze mwaka uliojengwa Msikiti, waliojenga msikiti kamani Mfadhili au waumini wenyewe. Ainishe kama msikiti unasaliwa Ijumaa au hausaliwi Ijumaa.

Pia aeleze wastani wa watu wanao Sali katiak Msikiti huo, na sehemu  ya kusalia wanawake imo au haimo katika msikiti.

Na mwisho utajwe uongozi wa Msikiti kwa majina yao pamoja na namba zao za simu kama ifuatavyo:-

  1. Imamu Mkuu
  2. Msaidizi Imamu
  3. Muadhini
  4. Katibu na
  5. Mshika fedha

Barua hii ya ombi la usajili wa Msikiti ipitie kwa Sheha wa Shehia uliopo Msikiti huo na Sheha atoe barua ya ombi la usajili wa Msikiti yenye anuani ifuatayo.

Katibu wa Mufti,

Ofisi ya Mufti

P.O.Box 2479

Zanzibar.

Barua zote mbili ziletwe ofisi ya Mufti kwa kuomba kusajili Msikiti.

USAJILI WA MADRASA

Katiaka kusajili madrasa unafuata utaratibu kama ulioelezwa katika usajili wa  msikiti ispokua usajili wa Madrasa utaengeza mambo ya fuatayo.

  • Barua hii itaje idadi ya wanafunzi wote, idadi ya wanafunzi wanawake na wanaume.
  • Barua itaje masomo yote yanayo someshwa katika Madrasa hiyo, na inapendekezwa masomo yasipungue saba.
  • Barua iainishe uongozi wachuo pamoja na namba zao za simu.

Hatua au jinsi ya utaratibu wa Kusilimisha wasiokuwa Waisilamu

Zinatolewa huduma kwa walio silimu na wale wanaotaka kusilimu bure .Huduma hii ni ambayo haicheleshwi hata kidogo. Ndani ya nusu saa mwenye kusilimu anakabidhiwa tarjisi yake ya kusilimu. 

Utoaji na Uendeshaji wa Mafunzo ya Ndoa

Kwa vile ofisi ya Mufti imejipanga vizuri sana. Masomo ya ndoa yanatolewa bure ndani ya muda wa meizi miwili na nusu kwa siku za Jumamosi na Jumapili tu, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa sita mchana.

Fomu za mafunzo ya ndoa zinapatika Ofisi ya Mufti bure, muhusika atajaza fomu ya mafunzo ya ndoa na kuirejesha ofisini.

Na baada ya masomo vyeti vya uhitimu vinatolewa bure, ambavyo thamani yake  ni kubwa mno katika jamii.

Utoaji na Uendeshaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa Waalim wa Madrasa

Mafunzo ya madrasa kwa walimu wa Unguja na Pemba  yanatolewa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mufti Mkuu  wa Zanziba, mafunzo hayo yanatolewa bure.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea walimu uwezo wa namna ya kufundisha kwa kutumia njia za kitaalamu ili kuwepesisha upatikanaji wa elimu ya dini mavyuoni kwa  urahisi, aidha walimu wa madrasa wanapatiwa mbinu za kupambana na udhalilishaji hassa katika maeneo ya madrasa  na jamii iliyowazunguuka.

Mafunzo hayo ni ya miezi mine, hivyo kwa mwaka tutakua na mikupuo miwili.

Masomo yanayofundishwa ni pamoja na English talking, Arabic talking, Arabic methodology, religion methodology, psychology, fiqih, ahkamtajweed, na  akhlaq islamiyya.

Mwisho wa mafunzo vyeti vitatolewa kwa wale watakaofaulu mitihani yetu ya majaribio naya mwisho.

Siku na muda wa mafunzo, alhamis, ijumaa na jumamosi kuanzia saa saba kamili hadi saa kumi kamili.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na  kitengo cha usajili na utafiti katika ofisi ya mufti mkuu -zanzibar.