Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1992 kwa Amri ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa wakati huo Mhe. Dk.Salmin Amour Juma. Aidha, baadae ikaanzishwa upya kwa Sheria ya Mufti Namb. 9 ya mwaka 2001. Kabla ya kuanzishwa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar baadhi ya kazi za msingi zilikuwa zikifanywa na Mashekhe mbali mbali wakiwemo wale wa Msikiti Gofu, wakiwemo Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Fatawi bin Issa n.k ambao walikuwa wakitoa Fatwa mbali mbali, utatuzi wa migogoro na kutoa Miongozo mbali mbali kwa kadri ilivyohitajika kwa wakati huo. Ama kwa upande wa Serikali, Mahkama ya Kadhi Mkuu ilikuwa ikitumika kwa madhumuni hayo.
Wasiliana Nasi
- P.O.Box 2479, Unguja Zanzibar
- +255 777 483 627
- info@muftizanzibar.go.tz
- www.muftizanzibar.go.tz
- Staff Mail
Wasiliana Nasi Pemba
- P.O.Box 132, Gombani Mpya Zanzibar
- +255 777 849 650