The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Muundo wa Ofisi

MUFTI

Ni Mkuu wa Ofisi ya Mufti anayeteuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa mujibu wa Kifungu Nam. 4(1) cha Sheria ya Kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti Zanzibar ya Mwaka 2001.

Baraza la Maulamaa

Baraza la Ulamaa linaundwa kwa mujibu wa kifungu cha 3rl), (2) cha Kanuni za Baraza hilo, lenye jukumu la kumshauri Mufti. Baraza ambalo Mhe. Mufti ni Mwenyekiti, na litakuwa na wajumbe wafuatao: –

a) Sheikh mmoja katika kila wilaya atakaeteuliwa na Waziri mwcnye dhamana kwa kushauriana na Mufti.

b) Masheikh sita (6) watakaoingia kwa nafasi zao, ambao ni: –

i) Mhe. Mufti, Naibu Mufti,

ii) Kadhi Mkuu, Naibu Kadhi Mkuu,

iii) Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana,

iv) Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kiislam.

Idara na Divisheni katika muundo wa Mufti

Muudo ulioidhinishwa ni muundo wa idara mbili (2), zenye divisheni sita na Ofisi ya Uratibu Pemba. Maelezo ya mundo huo ni kama ifuatavyo: –

Idara ya Fatwa , Usajili na Utatuzi wa migogoro

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itahusika na majukumu ya msingi ya Ofisi ya utoaji wa fatwa, usajili, utafiti na utatuzi wa migogoro ya kidini baina ya waislamu na waislamu na waislamu na wasiokuwa waislamu na uwekaji wa kumbukumbu za mambo ya dini. Idara hii ina lengo la kutoa miongozo ya kidini na uifanya jamii iishi kwa amani.

Majukumu ya idara

i) Kupokea maswali, kuyafanyia utafiti na kuyatolea jawabu.

ii) Kupokea na kusikiliza kesi, migogoro na mashauri ya kidini na kuyatolea ushauri wa kisheria kuyapatia sulhu.

iii) Kuandaa na kutoa taaluma ya dini ya kiislam katika vyombo vya habari, msikiti na mikusanyiko mengine ya kidini au inayohitaji miongozo ya kidini.

iv) Kufanya tafiti kuhusu kadhia na mambo ya kiislamu, ili kukuza utamaduni wa kiislamu na kuishauri ofisi kuhusu mambo yenye maslahi na Zanzibar.

v) Kuweka takwimu na kumbukumbu za maswali na ntajibu, kesi, ‘mashauri pamoja na muhtasari, wa vipindi, makala, mada na tafiti, kisha kuziripoti kwa Wakuu wa Divisheni au Idara, kwa kila mwezi.

vi) Kuratibu usuluhishaji wa mgogoro wowote wa kidini unaotokea baina ya Waislamu na Waislamu na watu wa dini nyengine.

vii) Kuweka takwimu juu ya kesi na migogoro inayopokelewa, inayotatuliwa na inayoendelea kutafutiwa ufumbuzi.

ix) Kukagua vituo vya  kutunzia  kumbukumbu  za Fatwa  na kuhakikisha zipo Salama.

x) Kutambua na kutafuta kumbukumbu za Fatwa zilizotolewa kwa vipindi tofauti .

xi) Kusajip, kukagua na kuweka kumbukumbu  za misikiti, madrasa na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar na Kusimamia mienendo yake.

1)  . Divisbeni ya Fatwa na Utatuzi wa  Migogoro

Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa divisheni na itakuwa na majukumu yafuatayo: –

i. Kupokea maswali, kuyafanyia utafiti na kuyatolea jawabu.

ii. Kupokea nakusikiliza kesi na mashauri ya kidini na kuyatolea ushauri wa kisheria, kuyapatia suluhu.

iii. Kuandaa na kutoa taaluma ya dini ya kiislam katika vyombo. vya habarj., msikiti na mikusanyiko mengine ya kidini au inayohitaji miongozo ya kidini .

iv. Kuweka takwimu na kumbukumbu za maswali na majibu , kesi, mashauri pamoja na muhtasari wa vipindi, makala, mada na tafiti na kuziripoti kwa wakuu wa divisheni au idara kwa kila mwezi.

v. Kumshauri Mkurugenzi katika jambo lolote litakaloisaidia ofisi kutekeleza majukumu yake na malengo yake kwa ufanisi .

vi. Kuratibu usuluhishaji wa mgogoro wowote wa kidini unaotokea baina ya·Waislamu.

vii. Kuratibu usuluhishaji wa mgogoro wowote unaotokana na Waislamu na watu wa dini nyengine, kwa kushirikiana na viongozi wa dini zao.

viii. Kupokea kesi na migogoro mbali mbali ya kidini na kuitafutia ufumuzi.

ix. Kuweka takwimu juu ya kesi na migogoro inayopokelewa, inayotatuliwa na inayoendelea kutafutiwa ufumbuzi.

2. Divisheni ya Usajili na Utafiti

Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na majukumu yafuatayo: –

i. Kusajili,  kukagua  na kuratibu  shughuli za madrasa  na vyombo  vya kidini (Maahadi).

ii. Kukusanya taarifa na kuweka kumbukumbu na kuratibu shughuli za maktaba za kiislamu, mihadhara na masheikh.

iii. Kukagua na kupitia kumbukumbu za vitabu, vipindi makala na taarifa za mitandao na kumshauri ipasavyo Mufti na katibu wa ofisi ya Mufti kuhusiana na athari za vyombo hivyo na shughuli za kitaaluma.

iv. Kufanya utafiti kwa azma ya kutatua matatizo yaliyopo katika nchi ya zanzibar.

v. Kuongoza shughuli zote za Taaluma na tafiti zinazofanyika ofisini.

vi. Kusimamia mienendo ya Misikiti , Madrasa na Jumuiya za Kiislamu za Zanzibar.

vii. Kutoa ushauri na kufanya tafiti kuhusiana na kadhia na mambo ya kiislam kwa lengo la kukuza utamaduni wa kiislam au kuishauri ofisi kuhusu mambo yenye maslahi na Zanzibar.

3. Divisheni ya Taaluma na Daawa

Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa divisheni na itakuwa na majukumu yafuatayo:-

i. Kuratibu shughuli za kuamrisha mambo mema na kukataza mambo maovu .

ii. Kuratibu na kusimamia vipindi, mawaidha, makala, miorrgozo na mafundisho yanayotolewa na ofisi, kwa lengo la ulinganiaji.  

iii. Kuratibu uandaaji wa khutba i1i kugawanywa kwa makhatibu na walinganiaji wanaozihitaji na kuwekwa katika mtandao wa ofisi kuwanufaisha  wahitaji.

iv. Kuhamasisha amani na utulivu Zanzibar kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, Masheha, Wanafunzi wa Vyuo na Taasisi mbali mbali, Maimamu, Walimu wa Madrasa na viongozi wa dini mbali mbali.

v. Kuratibu usuluhishaji wa mgogoro wowote wa kidini unaotokea baina ya Waislamu na Waislamu na watu wa dini nyengine .

vi. Kuweka takwimu juu ya kesi na migogoro inayopokelewa, inayotatuliwa na inayoendelea kutafutiwa ufumbuzi.

4. Idara ya Utawala, Mipango na Rasilimali watu

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itahusika na utekelezaji wa majukumu saidizi yanayohusu utawala, utumishi na mipango katika Ofisi, ili kuiwezesha Ofisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Majukumuya idara

i. Kutoa huduma za kiutawala na uendeshaji.

ii. Kushughulikia masuala ya Rasilimali Watu kama vile Mafunzo, Upimaji Utendaji Kazi, Mkataba wa Utoaji wa Huduma, Mishahara na stahiki nyengine za Watumishi.

iii. Kuratibu uandaaji, utekelezaji na kufanya tathmini za kazi za Ofisi ya Mufti.

iv. Kutoa mwongozo na utaalamu wa uandaaji wa  mipango, viashiria vya utekelezaji (Key Performance Indicators) pamoja na taarifa za utekelezaji wa kazi za Ofisi.

v. Kuandaa mfumo na muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripofi za utekelezaji.

vi. Kukusanya taarifa mbalimbali, kufanya uchambuzi na kutambua masuala yanayo paswa kujumuishwa katika takwimu za ofisi.

vii. Kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na kutoa ushauri wa kitaalamu  katika utekelezaji wake.

viii. Kusimamia na kufanya tathmini za utekelezaji wa miradi, mipango, na programu mbali mbali na kutambua matokeo yake.

ix. Kuandaa Ripoti ya Utekelezaji Kazi za Idara na kuiwasilisha kwa Katibu wa Ofisi ya Mufti.

  1.    Divisheni ya Utawala

Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na majukumu yafuatayo:-

i. Kutoa tafsiri na kuhakikisha kuwa kanuni na sheria mbalimbali zinazoongoza Utumishi wa Umma na masuala ya kazi zinaeleweka na kutumika ipasavyo.

ii. Kuweka mazingira mazuri ili kukuza uhusiano mwema kazini na maslahi ya watumishi.

iii. Kusimamia masuala ya kiitifaki ya ndani ya Ofisi.

iv. Kutoa na kusimamia huduma zinazowezesha Ofisi  kuendelea  kufanya kazi zake za msingi kama vile ulinzi, usafiri, ukarabati, utunzaji wa majengo na mazingira ya ofisi, umeme na maji.

v. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa masuala ya maadili  kwa watumishi wa Ofisi.

vi. Kutunza  masjala  na kuhakikisha  kuwa zinapatikana kwa urahisi kila zinapohitajika.

vii. Kutoa huduma za kuchukua na kusambaza watendaji.

viii. Kuandaa  ripoti ya utekelezaji  kazi ya mwezi,  robo,  nusu  na mwaka mzima.

5.   Divisheni ya Rasilimali Watu

Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa divisheni  na itakuwa na majukumu yafua ayo:-

i. Kuandaa  mahitaji  ya  watumishi  na  kuratibu  ajira  za  watumishi, upangaji wa watumishi katika nafasi  mbalimbali,  kuthibitishwa  kwa watumishi, upandishaji vyeo na kuhamisha watumishi.

ii. Kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu (Human Resources Plan) na kuainisha mahitaji ya wataalamu  kwa mpango wa muda mrefu.

iii. Kushughulikia masuala ya mishahara ya watumishi na orodha ya malipo ya mishahara.

iv. Kuratibu utekelezaji wa Mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi, kufanya ufuatiliaji, kutathmini matokeo na kuandaa taarifa ya utendaji wa watumishi.

v. Kukumbusha na kusimamia maandalizi ya watumishi wanaojiandaa na·kustaafu na wale wanaoacha kazi.

vi. Kuandaa na kurekebisha Mpango wa Urithishaji wa Madaraka (Succession Plan) kwa Ofisi na kusimamia utekelezaji wake.

vii. Kuandaa mahitaji ya watumishi, kuandaa na kutekeleza mpango wa mafunzo na kuhakikisha mafunzo ya awali ya watumishi wapya yametolewa kwa wakati.

viii. Kuratibu utekelezaji na uzingatiaji wa Mkataba wa Huduma kwa mteja.

ix. Kuandaa ripoti ya utekelezaji ya mwezi, robo, nusu na mwaka mzima na kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Idara.

6. Divisheni ya Mipango na Takwimu

Divislieni hii itaongozwa na Mkuu wa divisheni  na itakuwa na majukumu yafuatayo:-

i. Kuratibu uandaaji na usimamizi wa bajeti ya watumishi na matumizi ya kawaida ya Ofisi .

ii. Kufanya uchambuzi wa takwimu zinazokusanywa na Idara na Vitengo vya Taasisi kwa ajili ya utayarishaji wa Sera, Mipango na ya Bajeti ya Ofisi.

iii. Kuandaa bajeti na mpango wa utekelezaji wa kazi za Ofisi.

iv. Kushajiisha, kuratibu na kufuatilia upatikanaji wa rasilimali fedha na vifaa ambavyo ni muhimu katika utendaji wa kazi za kila siku .

v. Kushirikiana na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali katika kutayarisha, kutafsiri na kusambaza taarifa za kitakwimu zinazohusiana na Ofisi ya Mufti.

vi. Kuanzisha na kuratibu miradi mbali mbali ya Ofisi.

vii. Kutayarisha nyenzo za ufuatiliaji.

viii. Kuandaa ripoti ya utekelezaji ya mwezi, robo, nusu na mwaka mzim na kuwasilisha kwa Mku rugenzi wa Idara.

7. Ofisi ya Uratibu – Pemba

Ofisi hii itaongozwa na Msaidizi Katibu wa Mufti kwa kushirikiana na Naibu Mufti na itahusika na majukumu ya kuratibu shughuli zote za Ofisi ya Mufti, Pemba.

7.1. Vitengo vinavyo jitegemea

Muundo ulioidhinishwa wa Ofisi ya Mufti, utakuwa na vitengo (6) vinavyojitegemea na vinavyowajibika moja kwa moja kwa Katibu wa Mufti, kama ifuatavyo: –

i. Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu

ii. Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma

iii. Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

iv. Kitengo cha Huduma za Sheria

v. Kitengo cha Fedha na Uhasibu

vi. Kitengo cha Uhusiano

7.1.2Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu

Kitengo  hiki kitaongozwa  na   Mkuu wa  Kitengo  na kitakuwa     na majukumu yafuatayo : –

i. Kutoa ushauri kwa Katibu wa Mufti juu ya mambo yanayohusiana na ukaguzi na hesabu za ndani.

ii. Kufanya ukaguzi wa hesabu ndani ya Ofisi .

iii. Kupitia na kusahihisha hoja za wakaguzi wa nje.

iv. Kuandaa, ripoti ya ukaguzi.

v. Kufanya ukaguzi wa vifaa chakavu.

vi. Kutoa ushauri juu ya mwenendo wa matumizi ya fedha za Ofisi .

vii. Kuandaa bajeti ya Kitengo ya kila mwaka.

viii. Kutayarisha na kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi za Kitengo.

ix. Kufanya kazi nyengine zinazohusiana  na  Kitengo kama zitakavyopangwa na Katibu wa Mufti.

7.1.3. Kitengo cha Ununuzi na Uendeshaji wa Mali za Umma

Kitengo    hiki   kitaongozwa     na    Mkuu    wa    Kitengo    na    kitakuwa   na majukumu yafuatayo: –

i. Kutoa ushauri kwa Katibu wa Mufti juu ya mambo yote yanayohusu manunuzi na uondoshaji wa mali za umma.

ii. Kukusanya taarifa kwa ajili ya kutayarisha mpango wa ununuzi.

iii. Kukusanya taarifa za mahitaji ya ununuzi.

iv. Kufanya ununuzi wa mahitaji ya Ofisi.

v. Kudhibiti daftari la taarifa za zabuni.

vi. Kukusanya taarifa za uandaaji wa mikataba ya ununuzi.

vii. Kuhifadhi  kumbukumbu  za ununuzi  na za uchakavu  wa  vifaa  na kuziwasilisha  kunakohusika.

viii. Kuandaa bajeti ya mwaka ya Kitengo .

ix. Kutayarisha na kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi za Kitengo.

x. Kufanya kazi nyengine zinazohusiana  na Kitengo, kama zitakavyopangwa na Katibu wa Mufti.

7.1.4 Kitengocha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo na kitakuwa na majukumu yafuata: –

i. Kutoa ushauri kwa Katibu wa Mufti juu  ya mambo yanayo husiana na teknolojia ya habari na mawasiliano.

ii. Kutayarisha na kusimamia mfumo wa taarifa za wafanyakazi wa Ofisi.

iii. Kutayarisha na kusimamia Tovuti ya Ofisi.

iv. Kuandaa na kusimamia mifumo ya mawasiliano ndani na nje ya Ofisi .

v. Kuhifadhi na kusimamia kumbukumbu, nyaraka na taarifa zote za Ofisi katika matukio ya kila siku.

vi. Kuandaa bajeti ya mwaka ya Kitengo.

vii. Kutayarisha na kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi za Kitengo.

viii. Kufanya   kazi  nyengine  zinazohusiana    na  Kitengo, kama zitakavyopangwa na Katibu wa Mufti.