The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Ujumbe wa Katibu Mtendaji

Nina furaha ya kukukaribisha katika tovuti ya Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar , tunatumai utapata habari zenye kuaminika na zilizo kamili zitakazo kupa muungozo kuhusu dira, dhamira, shughuli na lengo kuu la Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar .

Lengo kuu la tovuti hii ni kufikia miongoni mwa matarajio ya Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ya kutoa fatwa, miongozo ya kidini na kusimamia masuala yote ya kiislamu kwa mujibu wa Sheria ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Namba 4 ya Mwaka 2021. Tovuti hii inatarajia kuendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na mikakati  inayochukuliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar katika  utoaji wa miongozo ya kitaifa ya kiislamu, kuimarisha uadilifu, ubora na ufanisi katika utoaji wa fatwa, utatuzi wa migogoro na usimamizi wa masuala ya kiislamu.

 Ni matumaini yangu kwamba tovuti hii itakua ni bora na yenye kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, Nia yetu ni kuboresha tovuti hii kila baada ya muda ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma kwa wananchi wote wa Tanzania na wageni wandani na nje ya nchi.

Shukrani

KATIBU MTENDAJI

OFISI YA MUFTI MKUU

ZANZIBAR