The Grand Mufti's Office of Zanzibar

Majukumu ya Ofisi

 • Majukumu ya Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar yametajwa katika kifungu Nam. 9 cha Sheria ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ya mwaka 2001 kama ifuatavyo:-
 • Kutoa Fat-wa ya jambo lolote linalowasilishwa na wananchi kuhusiana na shauri ambalo linahitaji kuamuliwa
 • Kutunza kumbukumbu zozote za Fat-wa zinazotolewa na Afisi yake
 • Kusuluhisha mgogoro wowote wa kidini unaotokea baina ya waislamu
 • Kusuluhisha mgogoro wowote unaotokana na waislamu na watu wa dini nyengine kwa kushirikiana na viongozi wa dini zao.
 • Kuandaa na kudhibiti shughuli za utafiti za kidini ndani ya Zanzibar zinazoendeshwa na taasisi za serikali au watu binafsi au mtu yeyote na kutoa vibali kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na waziri
 • Kuandaa muundo wa taaluma ya Ulamaa ndani ya Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ambayo itajumuisha elimu ya dini kwa lengo la kuinua fani hiyo
 • Kuratibu na kusimamia matayarisho ya mihadhara, warsha, semina na shughuli nyengine za kiislamu
 • Kuratibu shughuli za vikundi mbali mbali vya kiislamu ndani ya nchi
 • Kuratibu na kusimamia shughuli za misikiti yote na vyuo vya Qur-ani Zanzibar na kutoa miongozo pale inapohitajika
 • Kutunza kumbukumbu za misikiti yote na maulamaa wa Zanzibar
 • Kuratibu na kutangaza rasmi kuonekana kwa mwezi mwandamo
 • Kuidhinisha wahadhiri wa Dini ya Kiislamu kutoka nje ya Zanzibar baada ya kuridhika na uwezo wao
 • Kudhibiti,na kuidhinisha uingizaji, usambazaji wa tafsiri mbali mbali za vitabu mbali mbali vya kiislamu
 • Kuthibitisha usajili wa Jumuiya za Kiislamu kwa mujibu wa Sheria Nam.6 ya 1995
 • Kufanya mambo yote yatakayoweza kutokea na kusaidia kufikia malengo ya Sheria hii.
 • Kufanya jambo lolote lililoagizwa na Sheria hii au Sheria nyengine yoyote au lililoagizwa na Waziri kwa mujibu wa sheria